KLYINN KUWASHTUA MASHABIKI WAKE!!

Mwanamuziki Jaquiline Ntuyabaliwe aka Klyinn hivi sasa yuko Studio za 41 Records akirekodi albam yake ya tatu ambayo hakutaka kuitaja wala kutaja nyimbo zake isipokuwa amesema itakuwa ni ya kushtukiza kwa mashabiki wake.
Klyinn aliipasha FULLSHANGWE kuwa mpango wake ni kurekodi albam hiyo hapa nchini na kule ulaya nchini Uingereza ambapo producer Farouk anayefanya kazi zake huko ndiye atakayefanya kazi hiyo, kwani kwa sasa wakati anaendelea kurekodi hapa nyumbani katika studio za 41 Records Producer Farouk yeye anaendelea kuweka mambo sawa mara atakapokuwa amekamilisha maandalizi mimi nitaelekea huko kwa ajili ya kurekodi nyimbo zingine nchini humo.
Ameongeza kuwa kazi kubwa aliyonayo mwaka huu kwenye programu yake ni kuandaa hiyo albam hivyo atatumia muda mwingi kushughulikia kazi hiyo mpaka atakapokuwa amekamilisha kurekodi lakini pia ameongeza kuwa anataka kuonyesha ubora zaidi katika kazi yake ya sasa ambayo ana imani itakuwa ni zaidi ya albam zilizopita.
Mwanamuziki huyo mwaka akiibuka mwaka 2007 na kutamba na albam yake ya kwanza iliyoitwa Crazy over you na mwaka uliofuata 2008 akatoka na albam nyingine ambayo iliwachengua mashabiki wengi wa muziki wa Bongo Fleva iliyokuwa ikiitwa Nalia kwa furaha. kaeni mkao wa kula wadau ngoja tusubiri.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment