MBUNIFU FATMA AMOUR AJA NA KAKAKUONA!!, "UNAVYOVAA NDIYO ULIVYO"

Mbunifu Fatma Amour akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa idara ya Habari Maelezo leo kuelezea maandalizi ya onyesho lake linalojulikana kwa jina la Kakakuona ambalo litakuwa na ujumbe usemao "Unavyovaa ndivyo Ulivyo" litakalofanyika Machi 7 ambayo inakuwa ni siku ya wanawake Duniani ambayo husherehekewa kila mwaka onyesho hilo litafanyika kwenye ukumbi wa Dar Live uliopo Mikocheni jijini.
Katika onyesho hilo kutakuwepo na Burudani mbalimbali kutoka kwa msanii kutoka Arusha Angeris, Simba Arts, Exel Music Band na Lips Entertainment, Wabunifu watakaoonyesha mavazi yao ni Gabriel Saktamole mavazi ya kimasai, Ras Mizizi mavazi ya Kiafrika na Fatma Amour mwenyewe atakayeonyesha mavazi mbalimbali aliyoyabuni ambapo kiingilio katika onyesho hilo kitakuwa 20.000.
Onyesho hilo limedhaminiwa na jarida la Exel, Dollywood, DTP, Vayle Spring JD Entertainment,Aqua Well Drill, Clouds Fm, Easy Finance,British Council Sofia Prodution na CXC Tours, katika picha aliyekaa kushoto ni mbunifu Gabriel Saktamole na nyuma ni wanamitindo kutoka Dollywood watakaoonyesha mavazi siku hiyo kwa picha zaidi shuka chini upate uhondo zaidi mdau.
Vazi hili limebuniwa na Ras Mizizi ambaye pia atashiriki kuonyesha uwezo wake katika kubuni mavazi ya kiafrika kama unavyoliona.

Hili vazi limebuniwa na mbunifu Fatma Amour ambaye ndiyo muandaaji wa Onyesha la mavazi linajulika kwa jina la Kakakuona litalkalofanyika tarehe 7 mwezi machi kwenye ukumbi wa Dar Live Mikocheni jijini.

mwanamitindo huyu akionyesha vazi la kiamsai lilibuniwa na Gabriel Saktamole kutoka Arusha.

Angeris akiimba akapera ya moja ya nyimbo zake ambazo ameziimba inayoitwa wewe leo katika mkutano na wanahabari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari maelezo huku mmoja wa waratibu wa onyesho la mavazi la kakauona Asma Makau akifurahia kwa pembeni.


waonyesha mitindo wakiwa wamevaa baadhi ya nguo za wabunifu Gabriel Saktamole, Fatma Amour na Ras Mizizi.

Kinda Chipukizi la muziki wa kizazi kipya lililoibuliwa na Bongo Star Search lilikiwa katika pozik si mwaingine huyu ni Angeris kutoka Arusha ambaye kwa sasa ana single zake mbili zinazokwenda kwa jina la wewe na myBoo. Msanii huyu atatoa burudani katika onyesho mavazi la kakakuona


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment