SERENGETI BREWERIES NA NMB WAITAKATISHA TAIFA STARS, WAMWAGA VIFAA VYA MAMILIONI!!

Hii sanamu inaonyesha jinsi unadhifu wa wachezaji wa timu yetu ya taifa Taifa Stars utakavyokuwa watakapokuwa wakisafiri kesho huku wamevalia nguo hizi ambazo zimetolewa na makampuni mawili yanayoidhamini timu hiyo ambayo ni Serengeti Breweries Ltd (SBL)na National Microfinance Bank (NMB)vifaa vya michezo vilivyotolewa na kuikabidhi timu ya taifa ambayo ianondoka kesho kuelekea Ivory Coast ni suti nyeusi, tracksuits, mashati, tai zenye rangi za bendera ya taifa, viatu vya kuchezea na vya kutokea, jezi na bukta, mabegi ya safari, sandals na vifaa vingine vingi, vifaa hivyo kwa ujumla vina thamani ya shilingi milioni 70 ambapo kila kampuni imetoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 35. FULLSHANGWE inawashukuru wadhamini hawa wa timu ya taifa kwa kuivalisha vizuri na nina imani huko waendako watatuwakilisha vyema katika mashindano hayo mungu ibatiki Taifa Stars, Mungu ibariki Tanzania Yetu.
Katibu mkuu wa shirikisho la mpira nchini Fredirick Mwakalebela kulia Tedy Mapunda Afisa uhusiano SBL, Shadrack Nsajigwa mchezaji wa timu ya taifa Taifa Stars na Afisa mwanadamizi wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NMB Imani Kajula kwa pamoja wakizindua rasmi nguo za wachezaji wa timu ya Taifa watakazokuwa wakivaa wanapokuwa safari katika mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani yatakayoanza kutimua vumbi nchini Ivory Coast hivi karibuni.
karibuni makabidhiano yamefanyika leo kwenye Hoteli ya New Africa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment