NGWEAIR KUMWAGA (NGE 1982) MTAANI KAENI CHONJO!!

Ngweair akipozi na vimwana mbele ya Camera ya FULLSHANGWE katika Hoteli ya Movenpick imetulia hiyo mdau.
Add Image
Msanii wa siku nyingi na mwenye mistari ya kusisimua katika nyimbo zake anayejulika kwa jina la kisanii kama Ngweair amesema wapenzi wamuziki na mashabiki wake kwa ujumla wakae mkao wa kushangweka kutokana na makamuzi aliyoyafanya katika albam yake mpya inayoitwa Nge 1982 ambayo ina nyimbo kumi na tatu.

Ngweair aliyasema hayo wakati akizungumza na Tovuti ya FULLSHANGWE katika Club ya usiku Billicanas wakati alipojimuvuzisha kwenye club hiyo ili kupata shangwe za Serengeti Out of Africa Night hivi karibuni, usiku unaofanyika kila siku ya jumatano na burudani kutolewa na Vijana wa Masauti Akudo Impact.

Ngweair amesema katika albam hiyo kuna nyimbo kama Nipe dili masela ambao umebamba kisawasawa katika anga za Bongofleva, Birthday, 120, Mafia, A.K.A mimi, Bata kila sehemu, Bila muziki, Wanadata, Mapenzi gani, Mwambie ukweli, Singida Dodoma, She Parformes na Maua ya Msujo ambazo amezirekodi katika studio tofauti tofauti.

Msanii huyo machachari amezitaja studio hizo kuwa ni Bongo Records, 41 Records, Heryn B. Records na Kama Kawa Records zote za jijini, katika nyimbo hizo pia ameeleza kuwa amewashirikisha wasanii kadhaa mahiri katika muziki wa bongofleva ambao ni TID, Jay Moe, Bushoke, Lady Jay Dee, na wasanii wa Chemba Squard ambalo ni kundi lake.

Hii itakuwa ni Albam ya pili kwa msanii huyo ambapo albam yake ya kwanza ilikuwa ikiitwa AKA mimi aliyoitoa miaka mitano iliyopita ambayo nayo ilifanya vyema katika soko la muziki wa Bongofleva hivyo kumpatia umaarufu mkubwa na kupata mialiko mingi ya kufanya maonyesho mengi katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Ngweair anamalizia kwa kusema matarajio yake ni makubwa katika albam hii mpya ambayo anatarajia kuisambaza katika vituo vya rdio na televisheni kuanzia mwezi wa tatu kwani tayari amefanya pia video za nyimbo mbili Nipe dili na 120 ambao amemshirikisha msanii Chid Benz huku watengenezaji wa video hizo wakiwa Visal Lab Production.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment