Tanzania yakopeshwa bilioni 173.8 na Korea


Habari na picha Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salam.



Jamhuri ya Korea imetiliana saini na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya kuikopesha shilingi bilioni 173.8 ( Dola la Kimarekani milioni 124) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mitatu ya maendeleo hapa nchini.




Sherehe hizo zilifanyika jana jijini Dar es salaam na kuwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah kwa niaba ya Tanzania na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mheshimiwa Young-hoon Kim. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Khijjah, fedha hizo zitasaidia ujenzi wa upanuzi wa Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili(MUHAS) katika eneo la Mloganzila, usambazaji wa umeme katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na usambazaji wa maji katika Manispaa ya Dodoma.





Alisema kuwa katika mradi wa maji katika Manispaa ya Dodoma utagharimu shilingi bilioni 69.5 na utahusisha ujenzi wa vyanzo vya maji , ukarabati wa matenki ya kuhifadhia maji na ujenzi wa matenki mapya. Khijjah alisema kuwa kwa upande wa upanuzi wa MUHAS jumla ya shilingi bilioni 69.3 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa kufundishia na eneo la kutolewa matibabu.




Pia mkataba huo unalenga kusaidia kuboresha huduma ya umeme katika baadhi ya eneo la mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ambapo mradi huo utagharmu shilingi bilioni 35.




Aliongeza kuwa Dola milioni 18 zitasaidia vituo vya ufundi stadi katika katika mikoa ya Dar es aalaam , Pwani, Lindi na Manyara na Dola milioni 25 zitasaidia ujenzi wa daraja la Maragarasi.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment