SIMBA NA EXPRESS YA UGANDA ZANOGESHA TAMASHA LA SIMBA DAY UHURU!!

Naibu Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na waziri wa Habari utamaduni na Michezo Juma Ally Shamhuna akipokea jezi yake kutoka kwa Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage aliyopewa kama zawadi kwenye tamasha la Simba Day linalofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jioni hii jijini Dar es salaam ambapo tayari Simba na Express ya Uganda ziko uwanjani kwa mpambano wa kirafiki matokeo zaidi tutawapa baadae.
Naibu Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo wa serikali hio Juma Ally Shamhuna katikati Mwenyekiti wa klanu ya Simba Aden Rage kulia na Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe wakizindua rasmi jezi za timu ya Somba zitakazotumika nyumbani na Ugenini katika tamasha la Simba Day linaloendelea kwenye uwanja wa Uhuru.
Kikosi cha Timu ya Exipress kutoka Uganda nacho kikipasha.
Kikosi cha Simba kikipasha tayari kwa mpambano.
Twanga pepeta wakifanya vitu vyao mbele ya mashabiki wa simba jukwaa la kijani.

Mc wa tamasha la simba mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kutoka redio Clouds Ephraim Kibonde kushoto akiwa na msemaji wa klabu ya Simba Cliford Ndimbo katikati pamoja na waandishi wengine kwenye uwanja wa uhuru katika tamasha la Simba Day.
Mmoja wa viongozi wa kundi la marafiki wa simba Zakaria Hanspope akisalimiana na aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Crescentius Magori na marafiki zake wengine wa kundi hilo.
Mashabiki kutoka kundi la marafiki wa simba Friends of Simba wakiwa wamekaa kwenye jukwaa kuu huku wakishuhudia tamasha hilo.






Rapa wa bendi ya African Stars anayekwenda kwa jina la Furgasom akiendesha baiskeli ya rafiki yake mlemavu ambaye jina lake halikupatikana mara moja Twanga Pepeta inatumbuiza katika tamasha la Simba Day leo.
Mashabiki mbalimbali wa timu ya simba wakiwa uwanja wa uhuru katika tamasha la Simba Day jioni hii.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment