PAKSTAN YAKUMBWA NA MAFURIKO NA KUPOTEZA ZAIDI YA WATU 900!!

Baadhi ya wahanga wakijiokoa kwa Mitumbwi kutokana na mafuriko hayo nchini Pakstani Picha kwa hisani ya Skynews.

Umoja wa mataifa umetahadharisha kwamba zaidi ya watu milioni moja wanahitaji msaada baada ya kukumbwa na mafuriko yaliyosanbabishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Pakstan kutokana na kimbunga kikubwa.



Watu zaidi ya 900 wamethibitishwa kufariki na mamlaka za serikali ya Pakstan. na makazi yao kuharibiwa kabisa katika jimbo la Kahyber- Pakhtoonkhwa, huku watu wengine zaidi ya milioni moja wakihitaji msaada wa kibinadamu kutokana na kuharibiwa kwa mali na chakula baada ya kusombwa na mafuriko hayo.



Ofisa wa majanga wa Latifur Rehman Said amesema utafutaji wa miili ya watu bado unaendelea na inaonyesha vijiji vyote vimesombwa na mafuriko hayo. ikiwa ni pamoja na mifugo na mazao ya vyakula.



Serikali ya Pakistan imetuma zaidi ya vikosi elfu 30,000 kwa ajili ya uokoaji na kuhudumia watu walionusurika katika mafuriko hayo makubwa ambayo yameacha wananchi wakihangaika huku na kule ili kujiokoa bila mafanikio.



Watu kadhaa walionusurika katika mafiriko hayo wamejihifadhi katika misikiti wakisubiri misaada ya dharura na mpaka sasa wahanga elfu 19.000 wameokolewa huku wengine 27.000 wakihofiwa kunasa kwenye mafuriko hayo.

(Habari na mashirika ya Kimataifa)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment