Marufuku ya mabomu hatari kuanza kutumika


Mkataba wa Kimataifa wa kupiga marufuku mabomu yenye kusababisha maangamizi makubwaunaanza kutumika rasmi hii leo.


Mabomu hayo yajulikanayo kama cluster yakilipuka hufuatiliwa na milipuko mingine kadhaa yenye uwezo wa kusababisha maafa katika maeneo makubwa.


Wanaharakati wanaopinga silaha hizo wanasema mabomu hayo kwa kawaida yanashindwa kulipuka na kubaki hivyo kwa miaka kadhaa , na hivyo kuwa hatari kwa raia kwa muda mrefu baada ya mapigano kumalizika.


Zaidi ya mataifa mia moja yametia saini mkataba wa kupiga marufuku matumizi ya mabomu hayo.


Lakini baadhi ya mataifa yenye nguvu duniani--kama vile Marekani, Urusi, Pakistan na Israel -- yamekataa kusaini mkataba huo, wakisisitiza kuwa silaha hizo kisheria zinaweza kutumika kwa shughuli za kijeshi. Habari kwa hisani ya http://www.bbcswahili,com/

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment