Mwenyekiti wa yanga LLOYD NHUNGA katikati,Katibu mkuu kushoto LAURENCE MWALUSAKO kushoto na Msema ji wa klabu hiyo LOUIS SENDEU wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika klabuni hapo iliyopo mtaa wa jangwani
Klabu ya YANGA imekili kufanya makosa ya kuwakata wachezaji wake watano kwenye usajili wake wa msimu huu wakati wangali na mkataba na timu hiyo.
Katibu mkuu wa klabu hiyo LAURENCE MWALUSAKO amesema hivi sasa timu hiyo inafanya mazungumzo na wachezaji hao ili kumaliza matatizo hayo ingawa tayari wachezaji hao wameshapeleka mashitaka hayo kwa shirikisho la soka hapa nchini TFF.
Wachezaji waliotemwa na YANGA, dakika za mwisho ingawa bado wanamkataba na timu hiyo ni mlinzi WISDOM NDLOVU toka MALAWI na JOHN NJOROGE toka KENYA wengine STEVEN MARASHI na ALLY MSIGWA.
Pia klabu hiyo imesema matatizo yote hayo yamechangiwa na TFF kufanya marekebisho ya kanuni za ligi kuu katika usajiri kufanywa kwa haraka mno hasa kuhusu kila klabu kuwa na wachezaji watano wa kigeni Source
0 comments:
Post a Comment