Mwenyekiti wa Chama cha wanafunzi wa Jimbo la Rorya (USARO) Bw. Martin Alex Owuor ambaye anasoma katika kitivo cha Sayansi ya Jamii Chuo Kikuu cha Dar es salaam akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati alipotangaza kufanyika kwa Mdaharo wa wana Rorya wote waliotangaza nia ya kugombea katika jimbo hilo unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 Agosti jimboni humo.
Mdahalo huo utakutanisha wasomi wa jimbo hilo kutoka vyuo mbalimbali katika jimbo hilo pamoja na wagombea wanaotarajia kugombea jimbo hilo, amesema mambo yatakayojadiliwa katika mdahalo huo ni Elimu, Afya na Ustawi wa Jamii, Maji, Miundombinu, Uwekezaji pamoja na mustakabali wa mapigano ya Kiukoo na wizi wa mifugo ambao umekithiri jimboni humo.
Amemaliza kwamba kuna wagombea ambao wameshaanza kujipitisha jimboni humo na kutangaza kwamba umoja wa wanafunzi hao (USARO)unawaunga mkono lakini Mwenyekiti huyo amesema wao hawamuungi mkono mgombea yeyote na kwammba lengo lao ni kujadili matatizo ya Rorya ili yaweze kutatuliwa lakini pia lengo lingine ni kupima uwezo wa waliotia nia ya kugombea katika jimbo hilo.






0 comments:
Post a Comment