PEACE LUMELEZI KUMVAA KABOYONGA JIMBO LA TABORA MJINI!!

Bw.Peace Isaac Abrahams Lumelezi akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo wakati alipokuwa akitangaza nia yake ya kugombea ubunge jimbo la Tabora kupitia chama cha Mapinduzi CCM amblo kwa sasa linaongozwa na Mh Kaboyonga.
Lumelezi alizaliwa mwaka 1966 Mei na kusoma elimu ya msingi katika shule ya Kipalapala mkoani Tabora na mwaka 1983 alijiunga na shule ya sekondari ya Ruvu mkoani Pwani na baadae alifauru na kujiunga na shule ya sekondari ya Tosamaganga mkoani Iringa.
Mwaka 1986 alijiunga na jeshi la kujenga taifa katika kambi ya Ruvu na kuhamishiwa kambi ya Luwa mkoani Rukwa ambapo alihitimu mafunzo hayo mwaka 1987 na kujiunga na chama cha mapinduzi Januari 5 1987 na kupewa kadi namba D . 557482 katika kambi ya JKT Ruvu.
Mwaka 1987 alijiunga na chuo cha uongozi wa maendeleo Mzumbe (IDM Mzumbe) ambako alihitimu Stashahada ya juu ya Uhasibu na usimamizimwa fedha katika Serikali za Mitaa mwaka 1990.
Bw Lumelezi amefanya kazi katika Tume ya Utumishi wa Serikali (TUMITAA) kama mhasibu na amesomea pia mafunzo ya Usimamizi wa fedha Serikali za Mitaa katika chuo cha Glasgow Uingereza lakini pia ametumikia Serikalini katika Halmashaur mbalimbali nchini.
Hivyo amesema anataka kusaidiana na wakazi wa jimbo hilo ili kusaidiana na wakazi wote wa jimbvo la Tabora na wabunge wa mkoa wa Tabora kwa ujumla ili kuhakikisha matatizo yetu yanatatuliwa kama vile Reli na Barabara zetu

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment