KUJUA KWETU KUKO VINYWANI ZAIDI KULIKO VITENDO KWA HERI MAXIMO!!

Aliyekuwa kocha Mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo, ameagwa rasmi usiku wa kuamkia leo katika hafla fupi iliyoandaliwa na TFF Msasani jirani na shule ya Feza jijini Dar es salaam. Katika hafla hiyo, pamoja na mambo mengine, Kocha Maximo alipewa zawadi mbalimbali ikiwemo ya kinyago alichopewa na Mwenyekiti Mtendaji wa kiwanda cha Serengeti, Jaji Mark Bomani.
Ni dhahiri kwamba kocha huyo atakumbukwa kwa kazi yake aliyoifanyia Tanzania japokuwa bado kuna wadau wa soka ambao wanasema hakufaya kitu ila tunaojua kusema asante tunasema Maximo amefanya kitu kikubwa katika soka letu lililokuwa la kichwa cha Mwendawazimu enzi hizo, na anastahili kupongezwa mpaka hapa alipotufikisha manake kuna methali inayosema "Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni"
Yote kwa Yote tunasema Watanzania tunajifanya tunajua sana mpira wakati kujua kwetu kuko vinywani zaidi kuliko vitendo na kama ndiyo hivyo basi tukubali kwamba hatujui jamani.
(Picha kwa hisani ya Mtandao wa GPL)
Aliyekuwa kocha wa timy ya taifa Taifa Stars akiwa katika picha ya pamoja na Meneja mkuu wa Uhusiano na Mwasiliano Teddy Mapunda wakati wa sherehe ya kumuaga kocha huyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo.

Kocha Maximo akiwa na baadhi ya wachezaji w timu ya taifa wakati wa sherehe ya kumuaga.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment