Usiku wa kuamkia jana ofisi za Global Publishers zilivamiwa! Mara baada ya uvamizi huo walimteka mlinzi na kumfunga kamba kisha kuondoka naye na kwenda kumtupa maeneo ya kurasini Temeke jijini Dar es Salaam hata hivyo askari huyo yuko chini ya ulinzi anaisaidia polisi. Kulikuwa na makundi mawili ya majambazi waliokadiriwa kufika ishirini, ambapo kundi la kwanza liliondoka na mlinzi huyo ambaye alifungwa plasta mdomoni na kamba mikononi na miguuni, kisha kundi la pili lilivunja mlango na kuingia ndani ya news

room.
Walipoingia ndani ya news room walipekua na kuvunja droo kadhaa na kutupatupa vitu vingi ikionesha kulikuwa kuna kitu au nyaraka fulani waliyokuwa wakitafuta, kwani hakuna hata kompyuta moja iliyoibwa wala kuguswa! Zaidi walichukua TV moja ndogo ya flat screen, iliyokuwa reception kwa sababu wanazozijua wenyewe na kuondoka nayo.
Ni jambo la kushangaza kwa kweli na kumshukuru Mungu kwa kutuepusha na usumbufu na hasara ambayo tungeipata kama wangebeba kompyuta. Tumeona ni bora tuwafahamishe wasomaji wetu wapendwa juu ya jambo hili ili muweze kujua kilichotokea siku ya leo ambayo imetufungua macho na masikio na kutufanya tuamue kuchukua hatua madhubuti ya kuimarisha ulinzi na usalama wa kampuni yetu.






0 comments:
Post a Comment