Mhe. Raynald Mrope mbunge Masasi asema EWURA ifutwe!!


Na Joseph Ishengoma MAELEZO, Dodoma

Mbunge wa Masasi mkoani Mtwara Mhe. Raynald Mrope ameiomba serikali kuifuta EWURA kwasababu imesababisha Taifa kukosa msaada wa shillingi bilioni 45 kutoka taasisi ya ORET ya Uholanzi.


Mhe Mrope amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akichangia Muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya madini ya mwaka 2010. Amesema, “awamu ijayo naoimba serikali iifute EWURA kwasababu haimsaidii mwananchi wa kawaida, badala yake iunde vyombo viwili tofauti, kimoja kishughulikie maji na kingine kihusike na umeme na gesi, kwasababu chombi kilichopo sasa kimesababisha Taifa likose hela za bure kutoka kwa wahisani.” Taasisi ya serikali ya Uholanzi (ORET) inayosaidia nchi zinazoendelea, mwaka 2006, ilitoa shilingi bilioni 45 kusaidia usambazaji wa umeme vijijini katika mkoa wa Mtwara.

Umeme huo ungesambazwa na kampuni ya ARTMUS inayosambaza umeme wa gesi kutoka mnazi Bay. Hadi mwezi Mei 31, 2010, EWURA haikutoa kibali kwa ARTMUS kusambaza umeme huo.

Kama EWURA wangetoa kibali, wananchi wa mkoa huo wangeunganishiwa umeme majumbani kwa gharama ya shilingi 60,000/ badala ya 475,000/ zinazotozwa na shirika la ugavi la umeme nchini TANESCO. Kwamujibu wa Mhe. Mrope, baada ya EWURA kushindwa kutoa kibali kwa ARTMUS kwa muda, taasisi ya ORET iliamua kusitisha msaada huo na kuchukua hela zake ili kuwasaidia wananchi wa maeneo mengine walio tayari kutumia vema msaada huo.


Mbunge huyo wa masasi ameitaja sababu nyingine ya kufutwa kwa EWURA kuwa ni chombo hicho kutowajibika moja kwa moja kwa waziri mwenye dhamana ya nishati na madini. Hata hivyo sheria iliyopitishwa leo na bunge imefuta vipengele vilivyokuwa katika kipengele 41.6 ili kumpa mamlaka Waziri mwenye dhamana kuwa na kauli ya mwisho anapoona kuwa jambo Fulani lina maslai ya Taifa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment