Hatimaye Loyd Nchunga Ndiye aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa klabu ya Yanga baada ya kushinda kwenye uchaguzi unaoendelea ambao umefanyika kutoka siku ya jana na kuendelea mpaka usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa PTA viwanja vya Mwl. J.K.Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Wana FULLSHAGWE kwa njia ya simu Msemaji wa klabu hiyo Bw. Louis Sendeu amesema matokeo kamili bado hayajatangazwa lakini mpaka sasa kwa nafasi za mwenyekiti na makamu tayari wameshajulikana.
Amesema kwa upande wa Makamu Mweyekiti mfanyabiashara wa mafuta Davis Mosha ameibuka mshindi katika uchaguzi huo, lakini kinachoendelea sasa ili kukamilisha zoezi zima la uchaguzi huo ni kuhesabu kura za kamati ya utendaji zoezi ambalo bado linaendelea likikamilika taarifa zaidi zitatolewa.






0 comments:
Post a Comment