HABARI NJEMA JUU YA KWIKWI YA MTANDAO BONGO!!

Makao Makuu ya TTCL jijini Dar

Kwi kwi ya mtandao iliyokuwa inawakabili watumiaji wengi hapa nchini tangu siku ya Jumatatu imemalizika.

Kwi kwi hiyo ilisababishwa na kuharibika kwa kifaa kwenye kebo ya SEACOM inayopita chini ya bahari huko karibu na pwani ya Djibouti.

Wahusika wamefanikiwa kurejesha huduma kwa kupitia kebo tofauti kwa muda mpaka hapo kebo ya SEACOM itakaporejea hewani. taarifa kwa hisani ya michuziblog asante (ankal)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment