Wagombea watatu tayari mwameshapitishwa kwenda kwenye ngwe ya pili ya mchujo wa mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambapo mdau aliyepo mjini Dodoma anasema mkutano huo wa kumpata mgombea mmoja utaanza si muda mrefu kutoka sasa.
Hayo yamesemwa na Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mh. John Chiligati wakati akitangaza majina yaliyopitishwa kuingia ngwe ya pili ya kinyang'anyiro hicho mjini Dodoma ambapo amesema mkutano wa kamati kuu huo wa pili una
kazi moja ya kumpata mgombea wa urais Zanzibar.
Waliopitishwa na kamati kuu ya CCM kuingia ngwe ya pili ya kuomba nafasi ya kugombea urais visiwani Zanzibar ni Dr. Mohamed Ghalib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Ally Mohamed Shein pamoja naye Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha.
Mambo ndiyo hayo wadau tutapeana taarifa kadiri mambo yatakavyokuwa yakienda huko mji mkuu wa Tanzania.





1 comments:
Mimi ni mtu wa bara kwa hivyo sitapiga kura Zanzibar. Hata hivyo, ninachotaka kusema ni kuwa: kama mimi ningelikuwa Mzanzibari, ningelimpigia kura Dr. Shein. Kwa kipindi chote tangu awe makamu wa Rais, ameonyesha uchapakazi, uadilifu na kuwa si mtu wa vikundi wala majungu. Kwa kifupi, yeye ni mchapakazi mtendaji na si mwanasiasa wa maneno. Lakini siasa zetu za kiafrika zinaweza kufanya mtu asiye na uwezo wala uadilifu akapita na mtu mwadilifu na mchapakazi akaangushwa. Kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar natumai watampitisha Dr. Shein. Ngonyani, Kinondoni, DSM.
Post a Comment