Mwanamuziki Christian Bella wa bendi ya muziki ya Akudo Impaact amesema wamjiandaa vyeka ili kukonga nyoyo za mashabiki wao wakati wa onesho lao litakalofanyika kwenye ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma kekwa ajili ya kesho kwa ajili ya kutambulisha nyimbo zao mpya kama vile History no Change,Ndoa umefuria na Ubinafsi.
Amesema watakwenda Dodoma kwa ajili ya kutoa burudani kwa wakazi wa mji mkuu huo pamoja na wageni mbalimbali watakaohudhuria mkutano mkuu wa chama cha Mapinduzi utakaofanyika huko na kwamba wanamuziki wa bendi hiyo wamejipanga vyema na wako fiti kuwaburudisha wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake ambapo katika onesho hilo pia watatambulisha wanenguaji wao wapya.
Onesha hilo linadhaminiwa
na Kampuni ya CXC Africa, Blogu ya Janejohn5 na Blogu ya FULLSHANGWE.





0 comments:
Post a Comment