Aziz M. Abood ambaye ni mjumbe Halmashauri kuu ya CCM Morogoro Mjini (kushoto) akikabidhiwa fomu za kuomba kugombea ubunge katika jimbo hilo na Bw. Ali Issa Ali Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini katika ofisi kuu ya wilaya hiyo leo asubuhi.
Akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hizo Mh. Abood amesema ameamua kwa moyo mmoja na kwamba yuko tayari kuwatumikia wananchi wa jimbo la Morogoro mjini iwapo watampa ridhaa ya kuwaongoza na kwasemea katikamasuala mbalimbali kama vile Elimu, Afya, Uchumi na jamii kwa ujumla.
Amesema yuko tayari kuwasaidia akina mama, watoto na wananchi kwa ujumla wenye matatizo mbalimbali hasa katika elimu na afya lakini, pia akasema yuko tayari kuwasaidia katika suala la kiuchumi kwa kuhakikisha wanapata mikopo rahisi kupitia SACCOS mbalimbali zilizopo kwa kufuata taratibu na kanuni za kifedha ili kuwajengea uwezo kiuchumi na kuboresha kipato cha wananchi.
Mwana CCM Aziz Mohamed Abood akisalimiana na mwana CCM mwenzie Zahara Kitima wakati walipokutana katika ofisi kuu ya CCM Wilaya Morogoro Mjini wakati wa zoezi la kuchukua fomu za kuomba kugombea ubunge katika jimbo hilo.
ABOOD ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE MOROGORO MJINI!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment