WANYANGE WA REDDS MISS ILALA WALIPOVINJARI KATIKA CHUMBA CHA HABARI BUSNESS TIMES JANA!!

Washiriki wa kinyang'anyiro cha kumsaka Redds Miss Ilala 2010 walipotembelea ofisi za magazeti ya Business Times, Majira, Spoti starehe na Dar Leo jana ili kujionea jinsi uzalishaji wa magazeti hayo unavyofanyika.
Warembo hao walipata nafasi ya kujionea jinsi habari zinavyoanza kuandaliwa hadi kufikia kutoka zikiwa kwenye magazeti.
Warembo hao wanatarajia kupanda stejini siku ya jumamosi juni 26 kuwania taji hili kubwa kuliko yote kwa kanda ya Ilala ambapo mshindi atapata nafasi ya kuiwakilisha wilaya hiyo katika fainali za Vodacom Miss Tanzania 2010 zitakazofanyika badaye mwaka huu.
Picha kwa hisani ya
www.janejohn5.blogspot.com

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment