Benjamin Sawe
Maelezo Dar es Salaam
SHINDANO la kumsaka Redds Miss Ilala 2010 linatarajiwa kufanyika june 2010, mwaka huu. Akizungumza Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mratibu wa shindano hilo Bwana Kalikumtima, alisema maandalizi yanaenda vizuri na warembo 18 wanaotarajiwa kupanda jukwaani wapo kambini kujiandaa na kinyang'anyiro hicho. Alisema shindano hilo litafanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza na wana matumaini makubwa kwamba mshindi kutoka wilaya ya Ilala atakuwa ndiye Miss Tanzania 2010.
Bwana Kalikumtima alisema maandalizi yanaendelea vizuri licha ya msukumo mdogo kwa wadau wa urembo kujitokeza kununua tiketi za kuingilia ukumbini ili kujionea shindano hilo.
Akizungumzia zawadi, Bwana Kalikumtima alisema mshindi wa kwanza atapata kitita cha shilingi milioni 1,500,000 ambapo mshindi wa pili shilingi 1,000,000 na mshindi wa tatu atapata kitita cha shilingi 800,000.
Alizitaja zawadi nyingine ni shilingi 300,00 kwa mshindi wa nne na wa tano na washindi sita mpaka wa kumi watapata kiasi cha shilingi 150,000 kila mmoja ambapo washiriki waliobaki watapata kifuta jasho cha shilingi 100,000 kila mmoja.
Aidha alisema makampuni yaliyojitokeza kudhamini shindano hilo ni pamoja na Fullshangwe Blog,Redds Premium Original,Vodacom Tanzania,Channel Ten,Fabak Fashion,Habari na Daily News,Hoteli ya Lamada na Sophia Production.
Makampuni mengine ni Clouds FM,Valye Spring,Syscorp Group,Muzasha Tours and Safaris,USA Dars na Issa Michuzi.
Alisema shindano la kumsaka Redds Miss Ilala litaanza saa mbili usiku ambapo litasindikizwa na warembo wenyewe,kundi la wanne Star na bendi ya FM Academia ambapo wageni watapata nafasi ya kushuudia mechi zinazoendela za fainali za Kombe la dunia.
Pia bwana Kalikumtima alisema tiketi zinapatikana na zinaendelea kuuzwa shear illusion Mlimani City na Millenium Tower ambapo tiketi za daraja la kwanza ni shilingi 100, 000, daraja la pili ni shilingi 50,000 na tiketi za daraja la tatu ni shilingi 10,000.

0 comments:
Post a Comment