WADAU MBALIMBALI WASHUHUDIA SHINDANO LA REDDS MISS ILALA UBUNGO PLAZA!!

Hawa ni Warembo wa Miss Temeke kama kawa nao walipewa shavu la kuuza sura kwenye shindano la Redds Miss Ilala usiku wa kuamkia leo pale Ubungo Plaza kabla ya shindano lao litakalofanyika kwenye klabu ya TCC Sigara Chang'ombe Julai 9/ 2010, ambapo burudani itatolewa na kijana mahiri katika muziki wa bongofleva Banana Zorro na bendi yake ya B. Band lakini pia ikumbukwe kwamba siku hiyo kutakuwa hakuna mchezo hata mmoja wa kombe la dunia kwani itakuwa ni mapumziko hivyo ni wakati muafaka kwa wapendao burudani kuvinjari maeneo ya TCC Sigara ili kushuhudia shindano hilo,kwa sasa warembo hao wako katika mazoezi makali kwenye klabu hiyohiyo.
Jamani hawa ndiyo warembo wa Miss Kinondoni nao walikuwepo na wakapewa shavu la kuuza sura kabla ya shindano lao litakalofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, katika shindano hilo burudani itatolewa na kundi maarufu la THT na Sebene zito kutoka bendi ya African Stars, lakini pia kumbuka kwamba leo warembo hao watachuana katika kutafuta mshindi mwenye kipaji katika shindano la vipaji litakalofanyika kwenye Hotel ya Giraffe ocean view kule Mbezi Beach leo jioni.
Mdau Patcho Mwamba wa FM Academia kushoto akiwa na Queen Suzy wa African Stars kati na rafiki yao kama kawa walikuwepo katika kuwakilisha.
Wadau kutoka African Media Group wakifuatilia shindano hilo nao walidhamini kupitia kituo chao makini cha luninga cha Chanel Ten.
Mh! Mdau Nick Magarinza aka Nick But hakukosa kushuhudia kinyan'ganyiro hicho kama unavyomuona akiwa makini kufuatilia mdau.
Wadau ktoka Vodacom Tanzania nao walikuwepo, Vodacom ndiyo wadhamini wakuu wa Miss Tanzania.
Mkuu wa itifaki kamati ya Miss Tanzania Acle Albert Makoye kushoto, kaka Deo na Mdau Fred Ogot mwenyekiti wa kamati ya Miss Tabata kulia wakifuatilia shindano hilo.
Mamaa Asia Idarous na Mzee wa Hamsini nao walikuwepo.
Mdau Said Kilumanga kutoka Chanel Ten kushoto akifuatilia shindano la Miss Ilala lililofanyika usiku wa kuamkia leo Ubungo Plaza.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment