UTAFITI WA BIASHARA HARAMU YA WATU!!

Mtaalamu wa Utafiti kutoka chuo cha sayansi na Tiba kutoka Muhimbili Dar es Salaam (MUHAS) Dr. Switbert Kamazima (mbele kulia) jana jijini Dar es salaam katika warsha ya siku moja, akitoa Ripoti ya utafiti aliyoifanza kuhusu hali ya biashara haramu ya watu Tanzania. Ripoti hiyo imetolewa kwa wafanyakazi wa Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii chini ya mpango wa Taifa wa kudhibiti ukimwi. (NACP) ambapo imezitaja baadhi ya sehemu kuu za biashara hizo ambazo hutoa na kupokea ni Mikoa ya Iringa,Singida,Mbeya, Dodoma,Tanga,Shinyanga na Manyara. Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.
Dr. Edwin Mng`ong`o (kati ) Kulia) DR. Benett Fimbo. na (kush) Dr. Geoffrey Kiangi.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku moja kuhusu Hali ya Biashara Haramu ya Watu Tanzania. jana jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi jamii Dr, Edwin Mng`ong`o pichani hayupo.wakati wa ufunguzi huo. Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment