Mwanamuziki mwanzilisha wa Bendi ya African Stars Twanga Pepeta Ramadhan Masanja Aka Banzan Stone akiimba wimbo wa Kisa Cha Mpemba pamoja na Mwanamuziki na Kiongozi wa bendi hiyo Lwiza Mbutu leo kwenye tamasha la miaka kumi ya bendi hiyo lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam likihusisha maadamano ya amani, kampeni ya kupambana na Malaria inayosema Malaria Haikubaliki na michezo mbalimbali na kufuatiwa na burudani mbalimbali kutoka bendi za Msondo Music Band, mwanamuziki Mafumu Bilal Bombenga na Tony Nyadundo kutoka Kenya pamoja na African Stars yenyewe ambayo imepiga nyimbo zake kumi zilizopo kwenye albam zake kumi tangu ilipoanzishwa na kukonga nyyo za mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi katika kusherekea miaka kumi ya bendi hiyo..
Lwiza amesema Banza Stone ni kaka yake na walinza na bendi hiyo kwa hali ngumu sana mpaka hapo ilipofikia kwani wakati mwingine walikuwa wakitumia hata shuka moja kujifunika lakini ilkuwa wakilala kama kaka na dada.
Balozi wa kupambana na Malaria Joseph Haule aka Prof. J akiwaimbisha mashabiki wake hawapo pichani wakati alipokaribishwa mkutoa ujumbe wa kupambana na malaria kwa kauli mbiu ya
"Malaria Haikubaliki"
Mwanamuziki wa muziki wa asili kutoka nchini Kenya Tonny Nyadundo akionyesha uwezo wake wa kuimba na kupuliza kinanda cha mdomo wakati alipotambulishwa rasmi katika tamasha la miaka kumi ya bendi ya African Stars.
Haya wadau kazi kwenu hili ni kundi zima la wanenguaji wa kike wa bendi ya African Stars wakionyesha uwezo na uzoefu wao katika kazi yao hiyo.
Baba ni mahiri katika kupiga gitaa la sollo lakini mtoto anaimba, anaghani na anapiga gitaa la besi kwa ustadi mkubwa huyu si mwingine ni Kalala Junior kama mnavyomuona wadau.
Wanenguaji wa kiume kutoka Bendi ya African Stars wakionyesha uwezo wao katika kucheza miondoko ya kusugua kisigino.
Rapa mahiri wa Bendi ya Msondo Music Roman Mng'ande akionyesha umahiri wake katika kucheza kiduku moja ya staili iliyobukia kupendwa sana na mashabiki wa muziki wa taarab jijini Dar es salaam.
Dada Esther kushoto na Anna walikuwepo pia katika kushuhudia tamasha hilo kubwa la African Stars.
Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Leonidas Gama akizungumza wakati wa tamasha la maazimisho ya miaka kumi ya bendi ya African Stars yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders jiji9ni Dar es salaam wa pili kulia ni mkurugenzi wa ASET Asha Baraka na kushoto ni Mwenyekiti wa ASET Baraka Msilwa.
0 comments:
Post a Comment