Patrick Ochang mwenye miaka 24 na raia wa Uganda anacheza nafasi ya ushabuliaji na kiungo na viongozi wa simba walifanikiwa kumnasa baada ya kufuatilia uchezaji wake na kuridhika na kiwango cha mchezaji huyo na kwamba ni dhahiri kwamba ataisaidia sana timu hiyo katika mashindano ya kimataifa mwakani na ligi kuu ya Vodacom pia.
Wengene wanaoonekana katika picha ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu maarufu kama (Perez) aliyeko kushoto na kulia ni mmoja wa wanachama wa Simba kutoka Kundi la Friends of Simba Bw. Musleh mjumbe wa kamati ya usajili wakimkabidhi jezi mchezaji huyo.





0 comments:
Post a Comment