Rais Kikwete ziarani Mpanda azindua maabara ya kisasa,aweka jiwe la msingi mradi wa umeme, akutana na wazazi wa Waziri mkuu pinda!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua ujenzi wa mitambo mipya ya kuzalisha umeme mjini Sumbawanga jana asubuhi.Mitambo hiyo itauwezesha mji wa Sumbawanga na wilaya za jirani kupata umeme wa uhakika.Watatu kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja,wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO mhandisi Willoima Mhando na wane kushoto ni meneja mahusiano wa TANESCO Badra Masoud.
Mtaalamu wa Maabara katika hospitali ya mkoa wa Rukwa bwana Dodea Mlenda akimpa maelezo Rais Jakaya Mrisho Kikwete jinsi mashine mpya za kisasa za uchunguzi wa maradhi zinavyofanya kazi muda mfupi baada ya Rais Kuzindua maabara ya kisasa katika hospitali ya mkoa wa Rukwa jana asubuhi.Maabara hiyo ya hospitali ya mkoa wa Rukwa ni kati ya maabara 23 zinazojengwa katika mikoa mbalimbali nchini kwa msaada wa shirika la Abbott Fund lenye makao yake nchini Marekani.Kushoto ni Mbunge wa Kwela Chrisant Mzindakaya na watatu kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Waziri wa Afya Dr.Pamela Sawa.

Mama wa Waziri mkuu Alberina Kasanga akimzawadia kuku Rais Jakaya Kikwete wakati Rais alipowatemebelea nyumbani kwao eneo la Kibaoni,wilayani Mpanda,mkoa wa rukwa jana mchana.Kulia ni Mzee Xaveri Kayanza Pinda,Baba ya Waziri mkuu mizengo Pinda(picha na Freddy Maro)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment