MWANAIDI HASSAN WA JKT MBWENI NDIYE MCHEZAJI BORA WA MWAKA 2009!!

Mgeni rasmi katika tuzo za mwanamichezo bora wa mwaka wa chama cha waandishi wa habariza michezo TASWA ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la michezo nchini Kanali Idd Kipingu akimkabidhi tuzo yake mwanamichezo bora wa mwaka 2009 Mwanaidi Hassan ambaye ni mchezaji wa Timu ya Netball ya JKT Mbweni jana kwenye hafla iliyofanyika katika hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam baada ya kuwashina wenzake 11 waliokuwa wakiwania tuzo hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers Ltd.


wanaoshuhudia katikati ni mwenyekliti wa TASWA Boniface Wambura na kuanzia kulia kulia mchezaji wa michezo ya kutunisha misuli David Nyombo na Golikipa wa timu ya Simba Juma Kaseja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Breweriers Ltd Jaji Mark Bomani akimkabidhi tuzo yake golikipa wa timu ya Simba Juma Kaseja kulia ni Katibu mkuu wa TASWA Mgaya Kingoba na kushoto ni Mwenyekiti wa TASWA Boniface Wambura.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers Ltd Jaji Mark Bomani akizungumza mbele ya wanamichezo, waandishi wa habari pamoja na wageni mbalimbali walioalikwa kushuhudia utoaji wa tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka wa chama cha waandishi wa habari za michezo nchini TASWA jana kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Waddhamini wakuu wa tuzo hizo Serengeti Breweriers, mgeni wa heshima pamoja na viongozi wa chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA wakipiga picha ya pamoja na wanamichezo wote walioshinda tuzi mwaka jana 2009.
Duh wadau wakipozi kwa madaha mbele ya Camera ya FULLSHANGWE kutoka kushoto ni Dina Ismail Mahmoud a.k.a Mama Pipiro Tanzania Daima, Cesilia Radio Uhuru, baba mkubwa Masoud Sanani Busness Time, Teddy Mapunda Meneja Mkuu Uhusiano na Jamii Serengeti Breweriers ambao ndiyo wadhamini wa tuzo hizo, Angela Msangi TBC1 na mdau Suleiman Mbuguni a.k.a Mzee wa Harua.
Wanamuziki wa Kalunde Band wakiongozwa na meneja wa bendi hiyo Debora Nyangi kushoto wakifanya vitu vyao katika hafla ya tuzo za mwanamichezo bora wa mwaka wa chama cha waandishi wa habari za michezo nchini TASWA jana kwenye hoteli ya New Africa jijiniu Dar es salaam.
Mwanamuziki Sarafina Mshindo akiimba wakati wa onyesho la bendi yao ya Kalunde kwenye hoteli ya New Africa anayepiga Sollo kulia ni mwanamuziki Edson Alen.
Wadau wengine hawa ni kutoka New Habari kutoka kulia ni Rachel, Zaituni na Winniefrida.
Wakati nikipita huku na kule katika hoteli hiyo nikakutana na rafiki yangu mpedwa wa siku nyingi Bwana Godrey Kitundu kushoto akiwa na rafiki yake Kayanda Paul wakicheki gemu kati ya England na Algeria huku wakipata burudani kutoka bendi ya Kalunde.
Kutoka kulia ni Wadau Kambili wa Grobalpublishers Mwani kutoka New Habari pamoja na Ally Mkongwe wa ITV.
Baadhi ya waandishi na wanamichezo mbalimbali wakiwa katika hafla ya tuzo hizo kwenye hoteli ya New Africa jana jijini Dar es salaam.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment