Baada ya Mpiga solo Elistone Angai kutimuliwa kwenye bendi ya Mashujaa sasa moto umepamba baada ya jahazi la bendi hiyo kushikwa na mwanamziki Jado Field Force na kutoa wimbo matata unaoitwa "Safari yenye vikwazo" na wimbo huo kuchukua nafasi kubwa katika vituo vya redia mblimbali hapa nchini.
Mwanamuziki huyo ambaye amewahi kuimba katika bendi mbalimbali jijini Dare salaam anaonyesha uwezo wake katika kutunga nyimbo kutokana na ubora wa wimbo huo ambao umekua ukisikika mara kwa mara katika redio nyingi jijini na mikoani
Wimbo huo umrekodiwa katika studio za Malon Linche jijini Dar es salaam huku rapa ambaye ananogesha wimbo huo anakwenda kwa jina la Ibrahim a.k.a Mirinda Nyeusi, katika wimbo huo gitaa la sollo limpigwa na kijana Amos a.k.a Mkono wa Nabii.
Video ya wimbo huo imetengenezwa na kampuni ya NY Production chini ya King Dodoo la Bouche na tayari imeshaanza kusambazwa katika vituo mbalimbali vya redio jijini Dar es salaam hivyo itaanza kuonekana wakati wowote katika luninga, video hiyo pia inapatikana kwenye mtandao kupitia http://www.youtube.com/ kwa kuandika neno Mashujaa band alafu unabofya.






1 comments:
Mkuu, mimi naona kuwa mabinti hawa wanadhalilishwa na watu wanaowatumia katika show zao. Wamewaweka nusu uchi hadharani wakati wakijua kabisa kuwa hawapendezi hata kidogo. natumai wazazi, ndugu na jamaa zao hawafiki kwenye show hizo wakiona mabinti/dada zao wakijiweka katika hali duni namna hii. Au labda wao wanaona huu ndio "usasa" (modernity.) Dada zangu sisi wenyewe tujiheshimu kwanza kabla ya kutaka watu wengine watuheshimu. Aida.
Post a Comment