FRANCIS KIFUKWE AJITOSA KUWANIA URAIS WA KLABU YANGA!!


Ikiwa ni siku ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu za kugombe uongozi kwenye klabu ya YANGA ambapo uchaguzi umepangwa kufanyika Julai 18 mwaka huu,hadi sasa jumla ya wagombe 37 wamechukua fomu kuwania nafasi mbali mbali kwenye uchaguzi huo ambao wagombea wanne wanawania uwenyekiti na wengine wanne nao wanawania umakamu mwenyekiti kwenye klabu hiyo.
Wanaowania uwenyekiti ni pamoja na FRANCIS KIFUKWE aliyechukua fomu leo asubuhi, MBARAKA IGANGULA,EDGER CHIBULA na COSTANTIN MALIGO.
Wanaowania umakamu mwenyekiti ni AYUBU NYENZI,DAVIS MOSHA, ABED MOHAMED ABED na mwisho anaewania nafasi hiyo ya makamu mwenyekiti kwenye klabu hiyo ya YANGA ni mwenyekiti wa kamati ya Miss TANZANIA ,HASHIM LUNDENGA. Habari kwa hisani ya www.janejohn5.blogspot.com.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment