Jumla ya vyandarua milioni 5.1 vyagawiwa kwa wajawazito nchini!!



Jamal zuberi na Mwirabi Sise- Maelezo Dodoma


Jumla ya vyandarua milioni 5.1 vyenye viuatilifu nchini kote vimegawiwa kwa wanawake wajawazito na watoto.

Hiyo ni kutekeleza Sera ya Afya ya mwaka 2007 hadi sasa ambapo imesambaza kati ya idadi hiyo kiasi cha vyandarua milioni 13 vilisambazwa kwa watoto wachanga.

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda leo Bungeni wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo ya matumiszi ya fedha ya ofisi yake na ofisi ya bunge ya mwaka 2010/2011.

Alifafanua kuwa vyandarua milioni 5.6 viligawanywa kwa kila kaya yenye watoto wa umri chini ya miaka mitano bila malipo.

Alisema kuwa serikali ilinunua na kusambaza dawa mseto ya malaria kwa vituo vyote vya tiba vya umma vipastavyo 5,000.

Aidha kwa upande wa utoaji wa huduma za afya , Mhe Pinda alisema hospitali za mikoa zimeongezeka kutoka 17 hadi 21, vituo vya afya kutoka 382 hadi 468 na zahanati kutoka 3,292 hadi kufikia 4559 ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa huduma za chanjo.

"ujenzi wa hospitali ya magonjwa wa moyo muhimbili umeshaanza na inatarajiwa kukamiliak mwezi wa mei 2011 jambo ambalo itapunguza idadi ya wagonjwa wa moyo kwenda nje" alifafanua zaidi Mhe Pinda.

Hata hivyo alisema kuwa bado sekta ya afya inaupungufu wa watumishi ambayo inaadhiri zaidi vijijini ukilinganisha na mjini.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment