Mwezeshaji wa Mradi wa Champion kutoka Wilaya ya Kinondoni Bw. Mohamed Dimoso akiwauliza maswali watoto kuhusu mradi huo katika maadhimisho ya siku ya "Baba" yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya Bakhressa Manzese kwa upande wa wilaya ya Kionondoni Katika sherehe hizo ambazo mradi wa champion umeziadhimisha kwenye mikoa kumi ambayo shughuli za mradi huo zinafanyika kumefanyika matukio mbalimbali yakihimiza akina baba kujali na kutunza Familia zao na Kuvunja ukimya huku wakizungumza kwa kushauriana mambo mbalimbali yahusuyo familia zao katika kujikinga na maambizi ya ugonjwa wa ukimwi.Mikoa ambayo Championi imeadhimisha siku ya "Baba" ni Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Iringa, Mbeya, Tabora, Shinyanga na Mwanza huku katika jiji la Dar es salaam ikiadhimishwa katika wilaya zake zote tatu Kinondoni, Ilala, na Temeke.
George Saimon Mwenyekiti wa Kikosi kazi jamii Kinondoni katika mradi wa Champion kushoto akizungumza na Bw. Charles Werema Mwezeshaji, kulia ni John Solanya Mshindi wa Champion yaani "Baba" aliyeshinda katika tafiti za Champion kuhusu akina baba wanaojali familia zao pamoja na Barnabas Wandwi.
Kikundi cha ngoma za asili cha Kaole Sanaa Group kikitumbuiza katika maadhimisho hayo.
Wapingaji wa ngoma wakifanya vitu vyao
Wawezeshaji wakiweka sawa vipeperushi mbalimbali vyenye kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi na wanafamilia kuzungumza zaidi kuhusu mahusiano yao katika familia zao.





0 comments:
Post a Comment