TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA KWA WALIONUNUA ZAWASILI!!

Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Frolian Kaijage leo ameongea na vyombo vya habari na kusema kwamba tiketi za kombe la dunia kwa watanzania walionunua zimeshawasili ambapo shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limetuma tiketi 380 ambazo zilinunuliwa na watanzania.
Huku akionyesha tiketi hizo kwa waandishi wa habari Kaijage amesema kwa wale walionunua tiketi hizo wanatakiwa kwenda kuchukua wakiwa na risiti ili waweze kupatiwa tiketi hizo na baada ya kupatiwa tiketi hizo ili kupata viza katika ubalozi wa Afrika Kusini wanatakiwa kwenda na Tiketi ya ndege, tiketi ya kuingilia mpirani, Paspoti ya kusafiria pamoja na picha moja itakayotumika kwa utambulisho wa mhusika kwa usalama zaidi na taarifa mbalimbali wakati yuko katika fainali hizo endapo kutatokea lolote akiwa nchini Afrika Kusini
Wakati huohuo Rais wa Shirikisho hilo la TFF Reodger Tenga amesema bado wako kwenye mazungumzo na timu ya taifa ya Brazil ili iweze kuja hapa nchini kwa mchezo mmoja wa kirafiki na mara mambo yatakapokuwa sawa TFF itatoa taarifa zaidi juu ya ujio wa timu hiyo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment