
Meneja Mkuu wa Multchoice Tanzania Peter Fauel akizungumza wakati wa uzinduzi wa kombe la Dunia litakaoloonesha katika vituo vya televisheni vya SuperSport kupitia DSTV nchini Afrika Kusini, amesema katika michezo hiyo michezo 64 itaonyesha na mchezo mmoja utaweza kupigwa picha na kamera 32 hivyo watu wataweza kuona kila tukio litakalofanyika wakati wa michezo hiyo.

Meneja Mkuu wa Multchoice Tanzania Peter Fauel na TK kutoka Afrika Kusini wakipiga kifaa vifaa vya kushangilia vinavyoitwa Vuvuzela kama ishara ya kuhamasisha watu kushangilia kombe la Dunia huku kikundi cha ngoma cha Mchabwede Group cha Makumbusho kikitumuiza katika uzinduzi huo.

Wadau kutoka Maultchoice Levina Bandihai kulia Barbara Kambongi katikati na mdau kutoka Multchoice wakijisevia.

Meneja Uhusiano wa MultChoice Tanzania Barbara Kambongi kushoto, Cliton kulia na TK katikati kutoka SuperSport Nchini Afrika Kusini waliwakilisha pia katika Uzinduzi huo.

Wadau Nina Pocoloco kulia na Agnes Mnguto walihudhuria pia ili kushuhudia uzinduzi huo wa kombe la Dunia kupitia SuperSport.

Wakurugenzi wa Jambo Leo Juma Pinto Kulia na Beny Kisaka nao walikuwepo katika uzinduzi huo.

Kocha wa Yanga Kostadic Papic akitambulishwa na Mkurugenzi wa Jambo leo Beny Kisaka kwa Mgombea urais wa klabu ya Simba Aden Rage wakati wa uzinduzi wa kombe la dunia ambali litaonyesha na vituo vya Supersport kupitia DSTV.

Wadau mbalimbali wakiwa katika uzinduzi rasmi wa kombe la dunia kupitia Supersport ambapo televisheni hiyo itaonyesha katika chanel zake za Supersport michezo 64.
0 comments:
Post a Comment