SIMBA YATIKISA ZAWADI ZA LIGI KUU YA VODACOM LEO!!

Naibu Waziri wa habari Michezo na Utamaduni Joel Bendera akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Ligi Kuu yaVodacom iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo mara baada ya ligi hiyo kumalizika hivi karibuni na simba kuibuka kidedea kwa ktofungwa hata mchezo mmoja hivyo kuukwaa ubingwa huo kwa historia ya kipekee.
Waziri Bendera ameipongeza Simba kwa kuchukua ubingwa kwa staili ya aina yake lakini pia akapongeza vilabu vingine kwa kufanya vizuri katika ligi hiyo, ameongeza kwa kusema utawala bora na kufuata kanuni za mchezo wa soka ni kitu muhimu sana na si vizuri watu wa mpira kwenda mahakamani kutafuta kile wanachokiita kahi wakati kanuni zipo wanaweza kuzifuata na kupata haki zao.
Simba mbali ya kuwa mabingwa wa ligi ya Vodacom 2009-2010 imefanikiwa kutoa Kocha bora wa ligi, mfungaji bora na Kipa bora huku mchezaji aliyesaidia kwa uwezo wake wote timu yake akiwa Mrisho Ngassa wa Yanga.
Yanga imechukua milioni 15 huku timu ya Azam FC ikichukua zawadi yake ya milioni 10 na timu ya Africa Lion ikachukua shilingi milioni 5 kwa kuwa timu yenye nidhamu katika Ligi kuu ya Vodacom.


Necta Foya akizungumza wakati wa hafla hiyo.



Katibu Mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF akizungumza mbele ya wageni waalikwa waliojitokeza kushuhudia hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa ligi kuu
Imani Madega kulia Mwenyekiti wa timu ya Yanga akipokea mfano wa cheki ya shilingi milioni 15 kutoka kwa Naibu Waziri wa habari utamaduni na michezo Joel Bendera kushoto katikati ni mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru akizungumza katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera akimkabidhi mfano tuzo ya kiatu cha dhahabu makamu mwenyekiti wa Simba Omary Gumbo aliyopokea kwa niaba ya mchezaji Bora wa ligi kuu ya Vodacom Mussa Hassan Mgosi katika hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika leo kwenye hoteli ya New Africa.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment