NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
WANANCHI na wagombea viti mbalimbali katika uchaguzi wa mwaka huu ,wametakiwa kuielewa na kuizingatia sheria ya mpya ya gharama za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huo ufanyike kwa misingi ya demokrasia ya huru na haki.
Kauli hiyo, ilitolewa jana na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais na Utawala, Bora, Sophia Simba ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akizindua kampeni ya kitaifa ya uelimishaji wa umma kuhusu sheria mpya ya gharama za uchaguzi uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
“Ni muhimu wananchi na hasa wagombea na wapigakura kuielewa sheria ya gharama za uchaguzi. Pia ni muhimu kwa wapigakura kuzingatia sheria hii katika hatua za kuchagua wagombea ndani ya vyama na wakati wa kampeni za uchaguzi,” alisema Waziri Simba.
Waziri Simba alisema kwa kuielewa na kuizingatia sheria hiyo wagombea na vyama vya siasa wataweza kuwa wagombea halali wa vyama vyao na pia kepuka malalamiko kutoka kwa wapinzani wao.
Alisema sheria hiyo inataka wagombea kutaja vyanzo vya mapato na kutoa taarifa za matumizi kwa msajili wa vyama vya siasa katika muda unaotakiwa, kwani kutofanya hivyo ni kukiuka sheria na kunaweza kusababisha wagombea kutokuwa na sifa za kugombea.
Aliongeza kuwa serikali imejipanga vizuri katika kusimamia na kuitekeleza sheria hiyo, hivyo aliwataka wananchi kutoka ushirikiano ili iweze kufanikiwa.
Naye Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini, John Tendwa, akizungumzia kuhusu uwazi wa mapato na matumizi, ambapo alisema kwa mgombea wa kiti cha urais, anatakiwa kuwasilisha taarifa yake kwa Katibu Mkuu wa chama na ngazi ya ubunge na udiwani anatakiwa kuwasilisha taarifa yake kwa Katibu Mkuu wa cha cha siasa cha wilaya.
Alisema kila chama cha siasa kilichopokea michango inayozidi sh. milioni moja kutoka kila mchangiaji binafsi au sh. milioni mbili kutoka kwa kila taasisi kitoe taarifa kwa msajili wa vyama vya siasa. Pia sheria hiyo inataka fedha hizo zihifadhiwe kwenye akaunti maalum itakayofunguliwa kwa ajili hiyo.
Tendwa alisema hivi sasa uchambuzi wa kanuni za sheria hiyo unaendelea na wanatarajia kufanya kikao cha mwisho Aprili 6, mwaka huu na kuongeza kuwa elimu ya kwa wananchi kuhusu sheria hiyo itakuwainatolewa nchi nzima hadi siku moja kabla uchaguzi huo kufanyika.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, ambayo ni walimu wa utaratibu wa kutoa elimu ya sheria hiyo, Edward Lugakingira alisema mbinu mbalimbali zitatumika katika utoaji wa elimu kwa kuzingatia watu wasiojua kusoma na kuandika.
Alisema elimu hiyo iaanza kutolewa kwa awamu wiki moja baada ya uziduzi huo, kwani hivi sasa jopo la wataalum kutoka taasisi hiyo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) wanaandaa hadidu za rejea.
Lugakingira alisema elimu hiyo, itaanza kutolewa kwa awamu, ambapo mikoa sita ndio itakayoanza, ambayo ni Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Pwani, Morogoro na Dar es Salaam na itakayofuatia mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini.

0 comments:
Post a Comment