Mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan, Generali Scott Gration,ameanza mazungumzo ya dharura ya kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa mjini Khartoum, Sudan.
Madhumuni ya mazungumzo hayo ni kujaribu kunusuru uchaguzi wa kihistoria unaotarajiwa kufanyika mwezi huu, baada ya Mgombea rasmi wa chama cha upinzani, SPLM, Yasir Armani kujiondoa kwenye uchaguzi huo.
Kulingana na bwana Armani, hali ya sasa ya usalama katika jimbo la Darfur, inahujumu mazingira ya kufanyika uchaguzi huru na wa haki.
Wakati huohuo serikali ya Kenya imeelezea kukasirishwa na hatua ya mgombea wa chama rasmi cha upinzani SPLM, Yasir Armani, kujiondoa kwenye uchaguzi huo.
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Moses Wetangula, ameelezea kuwa Kenya inaamini kwamba vyama vya upinzani vinapaswa kushiriki katika uchaguzi huo ambao ni muhimu kwa mustakabli wa Sudan kusini.

0 comments:
Post a Comment