Rais Kikwete ampokea Waziri wa mambo ya Nje wa Ujerumani na kuongoza kikao cha NEC Karimjee!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Dr.guido Westerwelle(wapili kushoto) pamoja na Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani Bwana Dirk Niebel(kushoto) ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Mwenyekiti a CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya chipukizi wa CCM muda mfupi baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee ambapo aliongoza kikao cha Halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC).

Mwenyekiti wa CCm Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Zanzibar Amani Abeid Karume na Katibu mkuu wa CCM Bwana Yusuf Makamba wakiingia katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam tayari kuanza kwa kikao cha Halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC).

Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM NEC wakiwa katika kikao chao leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam(photo by Freddy Maro)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment