PRINCESS MAXIMA WA UHOLANZI AKUTANA NA WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI!!

Princess Maxima mke wa mtoto wa malkia wa uholanzi akijadiliana jambo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo leo juu ya uimarishaji huduma za kibenki kwa wananchi waliowengi. Princess Maxima huyo na ujumbe wake yuko nchini kwa ziara ya siku mbili ambapo atakutana na viongozi mbalimbali waandamizi wa serikali na taasisi za kifedha.
Princess Maxima akipokea zawadi ya vitu mbalimbali ikiwemo Kahawa, Chai na Korosho kutoka kwa Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo leo jijini Dar es salaam ikiwa ni ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania.
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. huyo sio malkia wa uholanzi!huyo hapo ni princess maxima mkee wa mtoto wa malkia uholanzi.malkia uholanzi anaitwa beatrix.


    mdau chaka zulu

Post a Comment