NGWEA KUCHINJA MBUZI VINGUNGUTI PASAKA!!


Msanii wa Kizazi Kipya Albart Mangwea (Ngweair), katika kusherehekea Siku kuu ya Pasaka, Jumatatu ya Pasaka patakuwa apatoshi katika Ukumbi wa Mpya na kisasa wa Mashujaa Pub, Uliopo Vingunguti Kiembe Mbuzi, ambapo kutakuwa na Shoo Kabambe itakayoambatana na Disco Kali litakaloshushwa na Madj wa siku nyingi(Wakongwe) –Dj Dullah, na Dj Say Dou.

Mratibu wa Shamrashamra hizo Said Salum alisema kuwa pia amewaandalia shindano la kukuza vipaji wasanii chipukizi( underground), katika muziki wa kizazi kipya ususani wakazi wa Vingunguti na maeneo ya jirani, Buguruni, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, na Tabata ambayo zawadi mbalimbali itatolewa kwa atakayeonyesha kipaji kuzidi wengine.

Alisema kuwa maonyesho hayo yataanza mapema ambapo zawadi ya kwanza itakuwa kwa mteja atakayekuwa wa kwanza kukata tiketi kuwa atapatiwa furana ya Mashujaa Musica ikiwa kama kumbukumbu ya Ukumbi wa Mashujaa Hall ambao ndiyo walezi wa Bendi hiyo.

Kiingilio kwa mujibu wa Said kitakuwa ni cha chini ili kukidhi uwezo wa vijana ambacho kimepangwa kuwa shilingi 3000 kwa wakubwa na 1000 kwa Disco Toto litakaloanza mapema saa kumi jioni hadi mbili usiku ambapo baadaye kitafuata Ngwea kuwapa raha mashabiki wake(kukimbiza kisanii) kabla ya kupisha Disco kwa watu wote kuserebuka.

Wakazi wa maeneo ya Vingunguti na majirani mmekaribishwa kufika siku hiyo kusherehekea Siku kuu ya Pasaka inayosherehekewa Takribani Dunia nzima ikiwa ni kukumbuka kuzaliwa kwa Kristo.

Ulinzi kwa ajili ya mazingira Said alisema kuwa umeandaliwa wa kutosha

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Huyu jamaa mjinga sana. Hivyo kupozi na sigara kilevi na ulimi nje ndio anaona ni "cool"? sisi tulioishi huko wakati tunasoma na kufanya kazi tunajua kuwa watu kama hawa kazi yao kuiga uchafu wa maghetto ya USA ambako wasichana wengi wanapata mimba wakiwa na miaka 13, 45% ya vijana kati ya miaka 16 na 25 wanatumia madawa ya kulevya, vijana wanauana wao kwa wao kwa ajili ya mihadarati na viatu vya Nike, watu hwataki kusoma, n.k. halafu eti sisi ndio tunawaona mfano wa kuigwa. Tuwacheni ujinga na ushamba huu. kuna mengi ya kuiga USA na Ulaya kama vile uchapakazi, usafi wa mazingira, matumizi mema ya kodi za wananchi, uwajibikaji n.k.

Post a Comment