Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amefuta ziara yake aliyopanga kufanya wiki ijayo mjini Washington ambako Rais Barack Obama anatarajiwa kuongoza mkutano wa kimataifa kuhusu Nuklia.
Netanyahu ameripotiwa kuchukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa Misri na Uturuki zilitaka kujadili mpango wa nuklia ulioanzishwa na Israel.
Israel haijakataa ama kukubali kwamba inamiliki silaha za nuklia na ni moja kati ya mataifa machache duniani ambazo hazijatia saini makubaliani ya kimataifa ya udhibiti wa silaha za nuklia.
Mkutano unaojumuisha zaidi ya nchi arobani, unalenga kutafuta njia za kuzuia kuenea kwa zana za Nuklia.

0 comments:
Post a Comment