Mkurugenzi wa Kampuni ya Mamaa Sakina Trans amewaandalia wakazi wa Vingunguti Burudani kabambe ya kukata na shoka kutoka katika kundi maarufu ya miondoko ya Taarabu Wana wa Jahazi chini ya mwanamuziki nyota wa Taarabu Mzee Yusuph katika shoo itakayofanyika katika ukumbi Mpya na wa Kisasa uliopo maeneo ya Kiembe Mbuzi Vingunguti siku ya tarehe 17 April 2010 Mamaa Sakina ambaye wengine wamezoea kumuita Cash Lady, alisema kuwa Onyesho hilo siku hiyo litakuwa ni la aina yake kutokana na maandalizi yanayoendelea kufanywa ikiwa ni pamoja na Mzee Yusuph kutambulisha nyimbo mpya pamoja na waimbaji wapya ambao amefanikiwa kuwaibua kutoka kwa wapinzani wake Zanzibar Stars.
Aidha Sakina amedai kuwa pamoja na yote hayo pia wakazi wa Vingunguti watarajie vitu vipya ukumbini ambapo manzari ya kupendeza ikiwa ni pamoja na viti maalum vimetayarishwa ili kuwawezesha wote watakaoingia kuketi nkatika hali ya usalama tofauti na siku zingine ambapo ameongeza kwamba vinywaji pamoja na vyakula vimetayarishwa vya kutosha ili kuwawezesha wote kupata chakula kutokana na mahitaji ya kikla mmoja.Jahazi Morden Taarab linaloongozwa na Mzee Yusuph.
katika kuhakikisha kundi hilo linawapa raha mashabiki wake wa Vingunguti, Jahazi Molden Taarab imejichimbia maeneo ili kujiweka sawa ambapo itaqshusha kikosi chote ikiwa ni pamoja na waimbaji wote akiwemo Aisha Abllah, na Mwanne Sekuru ambaye amebadili fani ya Uhandishi wa habari na kujikita katika anga za Taarabu.kiingilio mlangoni itakuwa ni shilingi 5000 kwa kila mmoja
0 comments:
Post a Comment