Chama cha Soka cha England-FA- kimesema kitatoa uamuzi iwapo waubadili uwanja wa Wembley ambao umekuwa ukilaumiwa sana baada ya michezo ya mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Tottenham Harry Redknapp alisema uwanja huo ni "fedheha" baada ya mchezo wao wa nusu fainali ya kombe la FA walipofungwa na Portsmouth siku ya Jumapili.

Siku ya Jumamosi, uwanja huo utatumika kwa mashindani ya mchezo wa raga baina ya Saracens na Harlequins.
Taarifa iliyotolewa na FA imesema "Mchezo wa soka unapewa umuhimu wa kwanza na tunaelewa ni wajibu wetu kutafuta njia ya kufanya uwanja huo uwe bora zaidi."
Nyasi za uwanja huo zimekwishatandikwa upya mara 10 tangu ulipofunguliwa baada ya kujengwa upya mwaka 2007.

Uwanja wa Wembley nyasi zake zinatunzwa na taasisi iitwayo Sports Turf Institute, iliyoajiriwa na Wembley National Stadium Limited, na gharama za kuweka nyasi mpya zinafikia paundi za Uingereza 100,000 .

0 comments:
Post a Comment