BUNGE LAHAMIA UKUMBI WA MSEKWA BAADA YA HITILAFU YA MFUMO WA SAUTI KATIKA UKUMBI MPYA!!

Spika wa Bunge Samwel Sitta akiingia kwenye ukumbi wa zamani wa Bunge wa Msekwa baada ya mfumo wa sauti wa ukumbi mpya wa Bunge kupata hitilafu Aprili 13, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Karatu, Dr. Wilbroad Slaa kwenye ukumbi wa zamani wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma, Aprili 13, 2010. Bunge lilihamia katika ukumbi huo baada ya mfumo wa sauti katika ukumbi mpya wa Bunge kupata hitilafu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Askari akihamisha joho la Spika kutoka kwenye ukumbi mpya wa Bunge kwenda kwenye ukumbi wa zamani wa Msekwa baada ya mfumo wa sauti katika ukumbi mpya Aprili 13, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Askari wakihamisha siwa kutoka kwenye ukumbi mpya wa Bunge kwenda kwenye ukumbi wa zamani wa Msekwa baada ya mfumo wa sauti katika ukumbi mpya Aprili 13, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia jambo katika mazungumzo kati yake na Mbunge wa Kwimba, Bujiku Sakila kwenye viwanja vyaBunge Mjini Dodoma, Aprili 13, 2010.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment