
Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkullo(katikati) akiwahutubia wakulima wa zao la mpunga wa Kijiji cha Mawemailo wilayani Babati juzi mara baada ya kutembelea scheme yao ya umwagiliaji yenye heka 900 mashamba ya mpunga. Waziri huyo aliwasisitiza umuhimu wa kuendeleza mshikamano wao waliouonyesha ili kuzalisha zao hilo kwa manufaa yao na Taifa. Wengine kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Babati Dkt Ian Langibori na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Emmanuel Kamba.

Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkullo(katikati) akisikiliza maelezo juzi kutoka kwa Mkulima wa Mpunga Mohamed Shaban(kulia) juu ya scheme ya umwagiliaji ya kilimo cha mpunga ya heka 900 katika Kijiji cha Mawemailo wilayani Babati. Wengine wanaosikiliza ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mercy Sila(kushoto). Waziri Mkullo alikuwa na ziara ya kutembelea mashamba hayo na kujionea shughuli za uzalishaji wa mpunga na pia kupata maoni kutoka kwa wakulima hao kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa zao hilo kupitia uwezeshaji wa Serikali. Picha na Tiganya Maelezo-Babati.
0 comments:
Post a Comment