Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya akizungumza na wataalam wa sekta ya maji (hawapo pichani) kutoka Halmashauri mbalimbali nchini wakati wa hafla ya kukabidhi magari 61 na Mashine za kudurufu 61 kwa halmashauri za mikoa 11 kusaidia Programu ya Maji na usafi wa mazingira vijijini leo jijini Dar es salaam.
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO.
SERIKALI imewatahadharisha Wakurugenzi wa Halimashauri nchini kutotumia magari yaliyotolewa kwa ajili ya Programu ya Maji na usafi wa Mazingira vijijini katika shughuli nyingine nje ya utaratibu uliowekwa.Hayo yalisemwa jana (leo) na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya wakati wa hafla fupi ya kukabidhi baadhi ya halimashauri magari 61, kati ya 125 na mashine za kudurufu 56 kati ya 171 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Magari hayo kila moja lina thamani ya sh. milioni 63.5 na mashine hizo sh. 460,000 kila moja yamekabidhiwa kwa halimashauri hizo ,kwa ajili ya kusaidia kutekeleza programu hiyo ili kuboresha huduma za maji nchini na kuinua maisha ya wananchi. Magari mengine yanatarajiwa kuwasili mwisho mwa Machi.“Napenda kuchukua nafasi hii kuwasihi mchukue dhamana ya kuyatunza magari haya. Mhakikishe yanatumika kwa malengo yaliyokusudiwa .Yasitumike kwa shughuli nyingine au shughuli binafsi. Msiuziane magari haya,”alisema Profesa Mwandosya.Waziri Mwandosya aliwaagiza kuwa wahakikishe wanayafanyia ukaguzi wa kiufundi magari hayo mara kwa mara na kwa wakati kama inavyotakiwa kupitia maelekezo yaliyomo kwenye vitabu husika.Aliongeza kuwa katika matengenezo na ukaguzi watumie karakana za halimashauri na kuwasiliana na kampuni ya Toyota wanapohitaji ushaur au maelezo ya kiufundi, huku watumie madereva wenye ujuzi na kuwataka wasiwadilishe mara kwa mara isipokuwa pale inapobidi.Tutawapatia nyezo za kufanyia kazi hakikisheni wananchi wanapata maji,” alisisitiza. Katika hafla hiyo Waziri Mwandosya alikabidhi magari manne za ambazo ni Biharamulo, Longido, Mpanda na Rorya.Waziri Mwandosya alizitaka mamlaka za maji kubaini vyanzo vya maji na kuvitunza.Alisema idadi ya watu wanaopata majisafi na salama kwa upande wa vijijini imeongezeka kutoka asilimia 53.5 mwaka 2004/05 hadi kufikia asilimia 61 kwa mujibu wa twakimu za Desemba mwaka 2009.Hivyo wanatarajia mwishoni mwa mwaka huu itakuwa ni asilimia 63, wakati malengo ya Millinea ya kuwapatia maji safi na salama wananchi wa vijijini ni asilimia 65 ifikapo mwaka 2010.Kwa upande wa miji ya mikoa makuu ya mikoa alisema idadi ya watu wanaopata maji hayo imefikia asilimia 84, lakini changamoto ipo Dar es Salaam ambapo wameweza kufikisha asilimia 68, wakati lengo la millinea ni kuongeza kutoka asilimia 73 hadi asilimia 90 ifikapo mwaka 2010.Waziri Mwandosya alisema ili kukabiliana na changomoto ni vema mipangomiji iende sambamba na huduma za maji na umeme.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya akimkabidhi funguo za gari Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Mpanda Injinia Godfrey Mbabaye.Takribani magari 61 na mashine 61 za kudurufu zimetolewa kwa Halmashauri za mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera,Kigoma, Mara,Tabora, Rukwa, Manyara, Mtwara, Arusha na Mbeya leo jijini Dar es salaam.
Wataalam wa sekta ya maji wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Wataalam wa sekta ya maji wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
0 comments:
Post a Comment