NA MAGRETH KINABO – MAELEZO KIBAHA
SERIKALI imetoa wito kwa wananchi wote kulinda na kuvitunza vyanzo vya maji na mazingira ili rasilimali hiyo iweze kuleta maendeleo ya taifa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Maji na Umwagilaji, Christopher Chiza wakati akigfungua maadhimisho ya 22 ya wiki ya maji yanaendelea kufanyika kitaifa wilayani Kibaha mkoani Pwani kwenye uwanja wa Mwendapole.“Ni lazima tukemee kwa nguvu vitendo vyote vinavyosababisha uchafuzi wa maji na mazingira na tusisite kutumia vyombo vya sheria vilivyopo kumchukulia hatua mtu yeyote atakayeonekana anasasababisha uchafuzi wa maji na mazingira,” alisema Naibu Waziri Chiza.
Naibu Waziri huyo alisema Serikali katika kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji vinatunzwa na kuhifadhiwa vizuri imetunga Sheria Mpya ya Utunzaji wa Rasilimali za Maji namba 11 ya mwaka 2009.“ Sheria hiyo inatoa maelekezo ya namna bora ya utunzaji na usimmamizi wa vyanzo vya maji.
Katikasheria hiyo ofisi za mabonde zimepewa jkumu kisheria kumchukulia hatua mtu au kiwanda kitakachosababisha uchafuzi wa vyanzo vya maji ua kuathiri mazingira,” alisisitiza. Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba, alisema vifaa vyenye thamani ya Dola za Marekani 6,500 katika mradi mpya wa maji vimeharibiwa kulingana na taarifa alizozipata juzi.“ Ninatoa wito kwa viongozi wa serikali za mitaa kuwa walinzi imara wa miundombinu ya maji, alisema Kihemba.Hata hivyo aliwataka wananchi kuepuka vitendo viovu vya uharibifu wa imundo mbinu hiyo.






0 comments:
Post a Comment