Polisi nchini Nigeria wanasema watu 49 watashitakiwa kwa mauaji, kufuatia ghasia za kijamii zilizosababisha mamia ya vifo vya watu.
Msemaji wa polisi Mohammed Lerama ameiambia BBC kuwa wengi wa watakaoshitakiwa ni Waisilamu kutoka kabila la Fulani.
Bw Mohammed amesema idadi ya watu waliokamatwa tangu kutokea kwa mauaji hayo katika mji wa Jos imefikia watu 200.
Polisi wanasema watu 109, wengi wao wakidhaniwa kuwa ni Wakristo, walikufa katika mapigano yaliyotokea siku ya Jumapili. Taarifa za awali zilisema idadi ya waliouawa ilikuwa zaidi ya 500.
Ghasia hizo zilifuatia mauaji yaliyochochewa na imani za kidini, karibu na mji wa Jos mwezi Januari, na kusababisha vifo vya watu 300, wengi wao wakiaminika kuwa ni Waisilamu. www.bbcswahili.com

0 comments:
Post a Comment