MATUKIO NA MISHEMISHE ZA KUTAFUTA NGAWILA JIJINI DAR ES SALAAM!!

Hii siyo safari bali ni mizunguko ya kutafuta riziki kama akina mama hawa kama walivyokutwa na Camera ya (Mwanakombo Jumaa wa Maelezo) maeneo TAZARA wakijaribu kupita huku na huko ili angalau waweze kujipatia chochote kwa ajili ya kujikimu kimaisha wao pamoja na familia zao.
"kweli mwanamke ni mama wa familia ukimuelimisha mwanamke umeelimisha familia".
Huyu ni kajana anayefanya kazi za uchuuzi wa biashara za mkononi katika misururu ya magari barabarani, wafanyabiashara kama hawa maarufu kama wamachinga wamekuwa wengi karibu katika barabara zote ambazo zinasifika kwa kuwa na misururu mirefu ya foleni jijini, mbinu yao hii wanayotumia kufanya biashara zao imekuwa ikihatarisha sana maisha yao kutokana na mazingira wanayofanyia biashara zao kuwa mabaya kwani wamekuwa wakipishana na magari kama mchezo wa kuigiza wakati wanapowafukuzia wateja kwenye magari ili angalau kuuza chochote walichonacho.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment