Washiriki wa shindano la Miss Pasaka wakicheza shoo ya ufunguzi katika mazoezi yao yanayofanyika kwenye ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa Azizi Ally jana jioni shindano hilo litafanyika wakati wa sikukuu ya Pasaka. Mmoja wa Waandaji wa shindano hilo Pendo Mwingira aka Mc Kibajaji amesema katika shindano hilo pia kutakuwa na onyesho la kutafuta kipaji linalotarajiwa kufanyika tarehe 18 Machi na mshindi atapata televisheni inchi 21 huku burudani ikitolewa na Five Star Molden Taarab kabla ya kufanyika shindano lenyewe hilo siku ya pasaka.
Zawadi zitakazotolewa kwa washindi katika shindano lenyewe zitakuwa kama ifuatavyo mshindi wa kwanza atapata kitanda futi tano kwa sita, wa pili atapata sofa seti na wa tatu Dresing Table.





0 comments:
Post a Comment