CHAMA CHA CCJ CHAKABIDHIWA HATI ZA USAJILI WA MUDA LEO!!

Msajili wa vyama vya siasa nchini Mh. John Tebdwa kulia akimkabidhi hati ya usajili wa muda mwenyekiti wa chama cha siasa cha (CCJ) Chama Cha Jamii Richard Kiyabo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za msajili wa vyama vya siasa jijini Dar es salaam, kushoto ni mwenyekiti wa chama hicho Renatus Muabhi, mara baada ya shughuli hiyo kufanyika John Tendwa alisema ni jambo la kujiuliza kwamba muda wa kusajili chama hiki mapema kabla ya uchaguzi ulikuwepo.
lakini sijui ni kwa nini hawakuanza mapema mchakato wa kuomba usajiri, hivyo kwa muda uliobaki kabla ya uchaguzi kufanyika hapo oktoba 25 /2010 ukijiuliza ni vigumu kuwahi kushiriki uchaguzi mkuu ujao kwani ili kuelekea uchaguzi huo kuna mambo mengi ya kujiandaa kwa upande wa tume ya uchaguzi na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ukizingatia kuwa ofisi hii haifanyi kazi ya chama kimoja tu cha CCJ.
Chama cha CCJ kitaweza kuomba usajiri wa kudumu baada ya miezi sita au kabla ya kukamilika kwa kipindi cha miezi sita na kama muda huo utakuwa umepita bila kufanya hivyo chama hicho hakitakuwa na sifa za kupewa usajili wa kudumu kwa mujibu wa sheria na kanuni za usajiri wa vyama vya siasa nchini.
Viongozi wa Chama Cha CCJ wakiteta kabla ya kukabidhiwa hati yao ya usajili wa muda katika ofisi za msajili wa vyma vya siasa leo kulia ni mwenyekiti Richard Kiyabo na katibu wake Renatus Muabhi.

Hapa wakiwa katika picha ya pamoja na msajili wa vyama vya siasa Bw. John Tendwa katikati kushoto ni mwenyekiti wa CCJ Richard Kiyabo na kulia ni katibu wa chama hicho Renatus Muabhi na mwisho kuliani nia Ludovick Joseph Lingia ofisa kutoka ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa.

Wanachama wa chama cha siasa cha CCJ wakiwa wamembeba juu juu mwenyekiti wa chama hicho mara baada ya kukabidhiwa cheti cha usajili wa muda wa chama hicho njem ya ofisi za msajili wa vyama vya siasa

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment